المدة الزمنية 2:7

MSIMAMO WA RAIS SAMIA KUHUSU CORONA - HATUWEZI KUKAA KIMYA, NITAUNDA TUME MAALUM

بواسطة Global TV Online
6 616 مشاهدة
0
29
تم نشره في 2021/04/06

MSIMAMO WA RAIS SAMIA KUHUSU CORONA - "HATUWEZI KUKAA KIMYA, NITAUNDA TUME MAALUM" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu amesema anatarajia kuunda kamati ya wataalamu ambayo itamshauri kuhusu hatua sahihi za kuchukua kuhusu ugonjwa wa #COVID19. Samia amesema hayo leo Jumanne, Aprili 6, 2021, wakati akihutubia taifa mara baada ya kuwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara aliowateua juzi na kusema kuwa Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa, na kwamba lazima ijulikane wazi kama inakubaliana na hatua za dunia au inazikataa. “Nakusudia kuunda Kamati ya wataalamu kuliangalia suala la Covid-19, waliangalie kwa upana wake, kuhusu tiba zetu, Tanzania sio kisiwa, lakini pia hatuwezi kukubali kila tutakacholetewa bila ya kufanya utafiti wa ndani. “Kamati ya Wataalamu wakae waliangalie kwa upana wake kitaalamu kisha watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha, ili tujue tunalikataa au kulikubali kwa Tafiti za kitaalamu, watupe upeo wa tatizo hili lilivyo na hayo yanayopendekezwa na ulimwengu. “Hatuwezi kujitenga kama Kisiwa na hatuwezi kupokea kila tunacholetewa, Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuwe na msimamo unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid-19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi haieleweki,” amesema Samia. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvonline ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506) ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2 ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 91