المدة الزمنية 4:2

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 3.3% HADI 3.6%.

بواسطة KAHAMA TV ONLINE
62 مشاهدة
0
1
تم نشره في 2021/07/08

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi Juni ,2021 umeongezeka hadi asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2021. Akizungumza na waandishi wa Habari leo Julai 8,2021 jijini Dodoma Kaimu mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu[NBS] Bi.Ruth Minja amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,2021 kumechangiwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula . Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka mfumuko wa bei ni pamoja na vitambaa vya nguo kwa asilimia 8.5%,nguo za wanawake kwa asilimia 6.3%,viatu vya wanaume kwa asilimia 6.2%,kodi ya pango kwa asilimia 4.9%,vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 5.6%,na gharama za malazi kwa asilimia 5.7%. Bi.Minja amefafanua mfumuko wa bei wa bidhaa za vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni ,2021 umepungua hadi asilimia 4.7% kutoka asilimia 4.9% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2021. Aidha,Bi.Minja ameainisha mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo ambapo nchini Kenya umeongezeka kwa asilimia 6.32% kutoka asilimia 5.87% huku nchini Uganda ukiongezeka pia hadi asilimia 2.0% kutoka asilimia 1.9%. Kaimu mkugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa amesema kuanzia mwezi huu ofisi hiyo itaongeza kuweka takwimu za uzalishaji wa umeme,saruji,mwenendo wa utalii,idadi ya watumiaji wa simu hiyo ni katika kurahisisha tathmini ya ufuatiliaji katika kutoa takwimu za muda mfupi kupitia tovuti. USISAHAU KU SUBSCRIBE CHANNEL YETU ILI UWE UNAPATA UPDATE MPYA KILA TUNAPO WEKA HABARI MPYA WAKATI WOWOTE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE MAANDISHI YA BLUU /channel/UCcCo ... https://www.instagram.com/kahamatvonline/ #KAHAMATVONLINE #HABARIZAHIVIPUNDE

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0